EKU FM — ELEWA KWA NINI UNAISHI
EKU FM ni jukwaa la redio na blog lenye ujumbe unaobebwa na jina lake:
E — Elewa
K — Kwa nini
U — Unaishi
Kwa pamoja, EKU maana yake ni “Elewa Kwa Nini Unaishi.”
Tunaamini kila mwanadamu ana thamani na kusudi la kuwepo duniani. Kupitia vipindi vya redio, habari, elimu, makala na maudhui mbalimbali, tunalenga kuelimisha, kuhabarisha na kufungua fikra, ili kumsaidia mtu kujitambua, kugundua yale asiyoyajua na kuelewa zaidi kusudi la maisha yake.
Dhamira yetu ni kufikia watu duniani na kuchangia kujenga jamii yenye watu wanaojitambua, wanaothamini maisha na kuelewa mapenzi ya Mungu katika maisha yao.
EKU FM — Elewa Kwa Nini Unaishi.
Si kuishi tu, bali kuelewa kwa nini unaishi.

0 Comments